Unknown Unknown Author
Title: MSANII JUMA NATURE KUOA MUARUSHA HIVI KARIBUNI, MSIKILIZE MWENYEWE AKIFUNGUKA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkongwe kwenye Muzuki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Juma Khassim Kiroboto Maarufu kama Juma Nature @Sir_Nature amesema Kuwa Siku za K...
Juma Nature
Mkongwe kwenye Muzuki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Juma Khassim Kiroboto Maarufu kama Juma Nature @Sir_Nature amesema Kuwa Siku za Karibuni Zijazo atamnuoa Mpenzi wake Ambaye anatokea Arusha.

Akifanya Mahojiano na DjHaazu wa Mambo Jambo Radio Arusha Tanzania, Juma Nature amesema kuwa amekaa bila Mke wa ndoa kwa kipindi Kirefu sana tangua aachane na alikuwa Mkewe ambaye Alibahatika Kuzaa Mtoto mmoja aitwaye FURAHA na kwa sasa anaamini ni Muda Muafaka wakufikia Hatua Nyingine ya Kuitwa Baba wa Familia.

Katika Mazungumzo hayo @Sir_Nature amesema pia kwamba Mwanaye Furaha anaishi na mama yake ila yeye kama Baba anamgharamia mwanaye Kila kitu ikiwa ni Pamoja na Shule Bora huku akisema kuwa yeye na Mzazi mwenzake huyo hawana Shida wako Sawa japo Mzazi mwenzake huyo alipata Bwana Mwingine na Kuolewa.

Katika Point nyingine Pia Nature amewaomba Mashabiki wake wakae Tayari kwani Karibuni anaachia Wimbo wake Mpya wenye Mahadhi ya Kwaito aliosema utaitwa GUSA UNASE.


Pia msanii huyu Tarehe 24/04/2015 ataweza kufanya show ya nguvu katika mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Bwalo la Polisi hivyo amewataka wapenzi wake kujitokeza kwa wingi iliwaje wapate burudani bora kabisa ambayo wameimiss kwa kipindi kirefu sana.

MSIKILIZE HAPA JUMA NATURE AKIONGEA NA DjHaazu

About Author

Advertisement

 
Top