Unknown Unknown Author
Title: MSANII HUYU MAARUFU AFARIKI DUNIA, KUZIKWA WILAYANI MASASI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za uhai wake. MAZISHI ya aliyekuwa msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao, 46, aliy...
 Chigwele Che Mundugwao
Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za uhai wake.

MAZISHI ya aliyekuwa msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao, 46, aliyefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya taifa Muhimbili, yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ado Novemba, alisema marehemu alifikwa na umauti huo baada ya kufikishwa hospitalini akitokea Keko gerezani ambako alikuwa mahabusi.
“Marehemu Che Mundugwao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu miezi miwili iliyopita, akiwa huko alipelekwa katika hospitali ya Amana na kugundulika na tatizo hilo. Mpaka sasa bado hatujafahamishwa chanzo cha kifo chake,” alisema Novemba.

Naye Makamu wa shirikisho hilo Samuel Mbwana alisema, “Che Mundugwao alilazwa katika hospitali ya Amana kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kurudishwa mahabusu na baadaye alipelekwa katika hospitali ya Muhimbili ambako alilazwa kwa muda kabla ya umauti kumfika leo saa moja asubuhi. Taarifa za mwisho za marehemu bado hatujazipata. Na ukizingatia alikuwa chini ya ulinzi hivyo bado hatujajua.”

Chigwele Che Mundugwao aliyekuwa ofisa Manunuzi wa Idara ya Uhamiaji na wenzake watatu walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mapema mwaka jana, wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo kosa la wizi wa Pasipoti 26.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahali panapostahili. Amina.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top