Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA AINGILIA GOGORO LA COASTAL UNION YA TANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Saidi katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na waliokaa akiwa kati...
Mgogoro Coast Union
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Saidi katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na Union, Steven Mguto,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

NA Mwandishi Wetu,TANGA
VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Saidi wakati alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana ambapo Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa viongozi wengine kwenye kikao hicho.

Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa ligi nyengine.

Mgogoro Coast Union
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Akida Machai akimuelezea mikakati ya timu hiyo mkuu wa Mkoa wa Tanga Magalula Saidi wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa Coastal Union na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana.

Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto alimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio.

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo iliyosalia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid Abdallah.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top