HABARI MUPYAA KUTOKA KWA MSANII SUMA LEE, AAGIZA NYIMBO ZAKE ZOTE KUTOPIGWA REDIONI NA WAZIFUTE KABISA

Kwenye Headline Ni mwanamuziki Suma Lee kukata Shauri na kuamua Kuacha Mziki, Aagiza Nyimbo zake zifutwe na Redio Wasizipige Tena
Suma Lee
Hit maker wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo na ameamua kusomea dini ya kiislam

Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.

“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia," Alisema Suma.

“Kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post