BAADA YA KUZUSHIWA KIFO MSANII HUSSEIN MACHOZI, HIZI NDIZO MSG ZILIZOTHIBITISHA UKWELI WA UHAI WAKE

Hussein Machozi
Leo hii Imeripotiwa kuwa Msanii Hussein Machozi amefariki Dunia Baada ya Kupata Ajali ya Gari, Taarifa hiyo imeedelea kuteka Baadhi ya Mitandao ya Kijamii pamoja na Blogs mbalimbali nchini Huku zikiambatanisha na Picha ya Gari hilo Pamoja na Picha Inayomuonesha mtu mmoja aliye jeruhiwa Vibaya sana Huku wakisema ndiye Hussein Machozi.
Post
Kufuatia Taarifa hizo Lindiyetu.com Ilihangaika kutafuta ukweli wa Habari Hiyo na ndipo ilipokutana na Post ya Msanii mwenzake wa Kizazi Kipya ajulikanae kwa Jina la H.Baba ambaye alitumia Fursa hiyo kukanusha taarifa hizo na kusema si za Kweli na yeye ameongea na Msanii huyo na yupo hai.
Lindiyetu.com imebahatika kupata chat msg ya Hussein Machozi na Mtu mwingine huku akionesha kushangazwa na taarifa hizo za kizushi, huku akitaka kujua ni nani aliesambaza taarifa hizo za Uongo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post