Unknown Unknown Author
Title: YANGA SC YAITUMIA SALAMU FC PLATNUM, BAADA YA KUICHAPA JKT RUVU 3 -1
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Yanga SC ya Tanzania imeitumia salamu timu ya Platinum FC ya Zimbabwe kufuatia ushindi mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Yan...
Yanga SC ya Tanzania imeitumia salamu timu ya Platinum FC ya Zimbabwe kufuatia ushindi mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga SC
Yanga SC imeifunga JKT Ruvu 3-1 katika ligi kuu Tanzania Bara, huku Danny Mrwanda, aliyewahi kucheza soka huko Vietnam akifunga goli moja na Simon Msuva akitupia mawili katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Hivi karibuni, Yanga pia iliwafunga Mgambo Shooting 2-0 ikiwa ni mfululizo wa ushindi katika mechi zake

Mechi hizo ni sehemu ya maandalizi kwa safari ya Yanga kuelekea Zimbabwe kurudiana na Platinum FC katika mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika mapema mwezi ujao.
Simon Msuva
Simon Msuva  Sasa awa kinara wa wafungaji katika ligi ya Vodoacom kwa jumla ya magoli 11 Akimpiku Didier Kavumbagu wa Azam FC mwenye Magoli 10.

Yanga ilishinda 5-1 katika mechi ya awali ikiwa uwanja wa nyumbani na inahitaji ushindi wa aina yoyote, droo au hata ikifungwa magoli yasiyozidi 4 ili isonge mbele kunusa hatua ya 16 bora.

Yanga kwa sasa inaongoza ligi kuu Tanzania Bara ikiwa a pointi 40 katika michezo 19 iliyocheza huku Azam ikifuatia ikiwa na pointi 36 katika michezo 18 iliyocheza.

Baada ya Mechi ya Leo, Ligi itaendelea tena hapo Aprili 4 kwa Mechi 5.

LIGI KUU VODACOM ::RATIBA:: Jumamosi Aprili 4

Mtibw Sugar v Stand United
Coastal Union v Tanzania Prisons
Ruvu Shooting v Ruvu JKT
Ndanda FC v Mbeya City
Kagera Sugar v Simba SC (Mechi kuchezwa Kambarage, Shinyanga)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top