Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi , OLIVER VAVUNGE
Wakizungumza na Lindiyetu.com wakazi wa vijiji hivyo wameelezea namna ukosefu wa barabara inayounganisha maeneo hayo umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbazi za kimaendeleo, ambapo pia wamesema kutokana na ukosefu wa huduma muhimu ikiwemo vifaa, na madawa muhimu katika Zahanati hiyo, inawalazimu kusafiri umbali mrefu hadi mjini kupata huduma hizo kwani mpaka sasa zahanati hiyo ina mtumishi mmoja tu anayehudumia wakazi wa eneo lote jambo linalohatarisha kwa kiasi kikubwa afya za wagonjwa hususani akina mama wajawazito pindi inapofika muda wa kujifungua.
Mganga wa zahanati ya Vijiji hivyo SOMOE RASHID amesema analazimika kufanya shughuli zote peke yake kutokana na kukosa wasaidizi ambao wamekuwa wakishindwa kuishi maeneo hayo kutokana na ugumu wa maisha ikiwemo changamoto kubwa ya ukosefu wa umeme na maji na hivyo kujikuta akifanya kazi peke yake na kukiri kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa katika Hospitali hiyo ambapo pia amesema uchakavu wa vifaa vilivyopo katika hospitali hiyo imekuwa changamoto kubwa inayokabili vijiji hivyo.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa Kijiji hicho AISHA LIPELA amesema changamoto za kijiji hicho zimekuwa zikiathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijiji hicho ambapo amesema kijiji hicho mpaka sasa hakina uongozi wa kuchaguliwa na wananchi jambo linalokwamisha jitihada za maendeleo katika eneo hilo.
Disemba mwaka jana wakazi wa vijiji hivyo waligoma kushirki katika zoezi la kujiandikisha wala kupiga kura kushinikiza serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa changamoto zinazo wakabili ambapo licha ya kufanya hivyo Hakuna jitihada zozote zilizofanyika.
Aidha wananchi hao wamelalamikia juu ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika zahanati zao za vijiji, jambo walilodai kwamba huathiri zaidi akina mama wajawazito inapofika wakati wa kujifungua.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.