AIBU TUPU: MKE WA MTU ASAULIA NGUO LAIVU LAIVU JUKWAANI WAKATI WA BENDI HII ILIPOTUMBUIZA

Lindiyetu habari
Na Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE mmoja anayedhaniwa kuwa ni mke wa mtu mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka kituko baada ya kupanda jukwaani na kusaula nguo zake mbele ya wanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ waliokuwa wakifanya makamuzi ndani ya Ukumbi wa Samaki Sport uliopo Kihonda mjini hapa.
Mbele ya umati mkubwa wa mashabiki walioingia ukumbini hapo kwa ofa ya mmiliki wa ukumbi huo, Farida Mees Matiou aliwaalika Twanga Pepeta kushiriki sherehe yake ya kuzaliwa sambamba na kuwataka mashabiki kununua bia mbili kama kiingilio, mwanamke huyo aliyeonekana amekolea kwa kinywaji, alivua nusu nguo mbele ya wanamuziki hao ambao baadaye uvumilivu uliwashinda na hivyo kuamua kwenda naye sambamba kwa kumkatikia mauno.

Baada ya kuona hali ya hewa inachafuka, kiongozi wa Twanga, Luiza Mbutu alilazimika kuzima muziki huku akiwashangaa wenzake kwa ‘kuwehuka’ na dada huyo.Baada ya kushuka jukwaani na kuulizwa sababu za kumwaga ‘razi’, mama huyo alimtaka mwandishi wetu kuachana naye kwani uwepo wake pale ulifahamika hadi kwa mumewe hivyo ‘asimkate stimu’.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post