Unknown Unknown Author
Title: RUBANI WA JORDAN AUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO NA KUNDI LA ISIS
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kuna video ambayo imesambazwa katika mtandao na kikundi cha kigaidi cha ISIS wakidai na kuonesha rubani mwenye asili ya JORDAN, MOAZ AL-K...
MOAZ AL-KASASBEH
Kuna video ambayo imesambazwa katika mtandao na kikundi cha kigaidi cha ISIS wakidai na kuonesha rubani mwenye asili ya JORDAN, MOAZ AL-KASASBEH akichomwa moto angali hai .

Ingawa mpaka sasa video hiyo haijathibitishwa ,inamuonesha mwanamume mmoja akiwa amesimama kwenye kizimba na anateketea kwa moto.

Video yenye kuonesha kisanga hicho iliachiliwa mtandaoni mwanzoni mwa wiki hii na kusambazwa katika mtandao wa Twitter, account ambayo hutumika kwa shughuli za kunadi matukio ya IS.

Luteni MOAZ AL-KASASBEH alikamatwa wakati ndege yake ilipokuwa ikitua karibu na Raqqa,nchini Syria mnamo mwezi December katika utekelezaji uungaji mkono majeshi yenye muungano na Marekani walioko kwenye mapambano na IS.

Nayo Runinga ya nchi ya Jordan imethibitisha kifo cha rubani huyo na kwamba alikwisha uawa mwezi mmoja uliopita.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top