Unknown Unknown Author
Title: MARKET PLACE YAINYUKA STAND WORIOUS 1-0, LIGI DARAJA LA TATU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Market Place yenye maskani yake Soko Kuu la Lindi leo hii iliikaribisha Timu ya Wapiga Debe ya Stand Kuu pia ya mjini hapa Lindi ...
Market Place Vs Stand Worious
Timu ya Market Place yenye maskani yake Soko Kuu la Lindi leo hii iliikaribisha Timu ya Wapiga Debe ya Stand Kuu pia ya mjini hapa Lindi katika Kipute cha Muendelezo wa Ligi Daraja la tatu ngazi ya Mkoa, Mchezo huo ulichezwa ndani ya Uwanja wa Ilulu.

Hapo jana Katika Mechi kati ya Beach Boys na Madson ya Nyangao iliisha kwa Timu ya Beach Boys Kuibuka kidedea kwa Magoli 3 - 0. Hivyo kwa ushindi huo wa Jana timu Hiyo ya Beach Boys ilipaa kileleni mwa Ligi hiyo na Kushika Usukani kwa Kujikusanyia jumla ya Magoli 4 na Point 4.

MCHEZO WA LEO,, Market Place Vs Stand Worious
Timu ya Market Place imeibuka kidedea katika Mchezo huu kwa Jumla ya Goli 1 - 0 Dhidi ya wapinzani wao wa Jadi Stand Worious.
Market Place Vs Stand Worious
MASHABIKI WA MARKET PLACE WAKISHANGILIA USHINDI HUO HUKU WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU JUU GOLKIPA WAO.....

Mpira huo uliweza kutawaliwa na Uchezaji mbaya wa Rafu nyingi ambapo refa alionyesha dhahiri kuto umudu Mchezo huo na kupelekea wachezaji kuchezeana ovyo, Ila mnamo Dakika ya 85 ya Kipindi cha Pili refa aliweza kumwadhibu Mchezaji wa Stand Worious Abdallah Saidi Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya Mchezaji wa Market Place na Kufanya Timu hiyo Kumaliza dakika 90 za Mchezo ikiwa Pungufu.
Market Place Vs Stand Worious
Refa akimuadhibu Abdallah Saidi Kwa Kadi nyekundu baada ya kufanya madhambi ya makusudi kabisa kwa kumpiga teke mchezaji mwanzake.....!!!

Aidha Chama cha Soka cha Lindi kimeshauriwa kuangalia tena upya uwezo wa Waamuzi wanaochezesha Ligi hiyo kwani kila siku zinavyozidi kwenda hali ya Maamuzi ya kimchezo ya marefa inakuwa mbaya.
Market Place Vs Stand Worious
Refa akisindikizwa na Maaskari katika chumba cha kubadilishia Nguo mara baada ya Kumaliza Mchezo wa Ligi daraja la Tatu kati ya Market Place Vs Stand Worious

akizungumza na Lindiyetu.com Shabiki mmoja amesema kuwa "Angalia Refa wa Leo huyu amechangia kiasi kikubwa kuvurugika kwa Mchezo huu, alishindwa kabisa kuumudu mchezo mchezaji anachezewa faulo lakini yeye ndio anapewa kadi ya manjano, Kosa lingine la dhahiri kabisa amewanyima penalty ya wazi Timu ya Market Place, Je kwa hali hii tutafika tunako kwenda?" Alimalizia Mdau huyo wa Michezo alietaka jina lake kutotajwa mtandaoni.
Market Place Vs Stand Worious
Wachezaji wa Market Place wakishangilia goli lao la kwanza na laushindi dhidi ya wapinzani wao Stand Worious uliochezwa leo katika Uwanja wa Ilulu.

Aidha Timu ya Market ilijipatia bao lake la Pekee na Laushindi Mnamo dakika ya 17 ya mchezo huo kupitia Mshambuliaji wake machachari Maiko Mlekela. Kwa matokeo hayo Timu hiyo inashika nafasi ya Pili ya Msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na Point 4 na Magoli 2 baada ya Kutoka Sare ya Goli 1 - 1 dhidi ya Transporter ya Kilwa hapo Juzi.

Kesho Ligi hiyo inaendelea kwa kuzikutanisha Timu za Madson Fc Vs Transporter katika Uwanja wa Ilulu.

VIKOSI VYA LEO:: Market Place:: Abdul Saidy Ally (gk), Onesmo S.Nguta, Amichael D.Mlekwa, Justin Simon Simao, Issa Kigaga, Sande M.Amani, Rocky Calte Michae, Rajabu S.Msela, Sultan Jagna, Mwalami I.Mahmoud, Hija Rajabu
Akiba::Saidi Mohamed Dadi, Ramadhani Rashid, Oktan Mbemba, Hussein Ndee, Saidy Mnende, Mohamed Mtaa, Ally Akika Pole
Stand Worious:: Chirston John Rotan (Gk), Mustafa Mohamed Mangana, Seleman Hussein Masha, Rupise Selemani Rupise, Silvester Pete, Abdallah Saidi Litanda, Emanuel Grayson Benge, Saidi a. Nyagaruka, Msafiri H. Kambwili, Joseph Hilly, Andrew Kariati
Akiba::Manuphed s.Rauma, Alfani Iddi Mussa, Ally Mussa Mtanda, Charles Tamba, Miliston Evalisto Malidadi, Saidi Maurid Mnongya, Hamisi Hussein Saidi

Market Place Vs Stand Worious
Mashabiki wakionekana kufuatilia kwa makini Mchezo huo uliokuwa ukichezwa ndani ya Uwanja wa Ilulu kati ya MarketVPlace 1 - 0 Stand Worious
Market Place Vs Stand Worious
Mashabiki wakionekana kusimama hii ni baada ya Mchezaji wa Stand Worious Kufanya faulo ya makusudi ya kumpiga teke mchezaji wa Market Place, Mchezo huo uliisha kwa Market Place 1 - 0 Stand Worious
Market Place Vs Stand Worious
Fouth Official akijaribu uwatuliza benchi la ufundi la Stand Worious ambao walikuwa wakimlalamikia refa kwa maamuzi yake..... 
Market Place Vs Stand Worious
Beki wa Stand Worious akijaribu kuokoa hatali iliyopo katika eneo la timu yake.......!! 
Market Place Vs Stand Worious
Kocha wa Market Place akiwatuliza wachezaji wake kuacha kupani na kucheza mpira hii ni baada ya kuona timu pinzani inacheza mpira wa rafu nyingi na bila ya muamuzi kuwaadhibu wapinzani......!!!
Market Place Vs Stand Worious
Fourth Official Akiandika baadhi ya mambo katika Ripoti yake ya Mchezo huo.....
Market Place Vs Stand Worious
Shabiki akitokelezea katika kamera zetu..Ila haikujulikana kama ni wa Timu gani...

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top