Unknown Unknown Author
Title: DIAMOND PLATNUMZ (@diamondplatnumz) KUTOA NYIMBO NNE MFULULIZO, KATI YA HIZO FALLY IPUPA NDANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwaka jana mwishoni (2014) baada ya Diamond kukutana na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo Fally Ipupa na P-Square nchini Nigeria, alisema...
Mwaka jana mwishoni (2014) baada ya Diamond kukutana na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo Fally Ipupa na P-Square nchini Nigeria, alisema “nikikutana na 18 huwa naachia bonge la shuti mpaka nishinde” na kauli yake imetimia. 
Diamond na Fally Ipupa
Staa huyo wa ‘Ntampata Wapi’ amefanikiwa kufanya collabo na staa wa DRC, Fally Ipupa ambayo ni miongoni mwa nyimbo nne alizopanga kuzitoa kati ya sasa na mwezi wa tatu.

Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kuwa wanampango wa kutoa nyimbo nne mfululizo hadi kufika mwezi wa tatu 2015, zikiwemo za Diamond na zingine alizofanya collabo na wasanii wa nje.

“Huu mwaka tunaugeuza vizuri kutoka January mpaka March tuna release nyimbo nne mfululizo ambazo ni za Diamond na zingine ni za watu wa nje ambao feauturing Diamond. Fally ametokea kumkubali Diamond, kwahiyo ngoma inakuwa ya Fally na Diamond, kila mmoja anafanya kwenye sebule yake tunakutana kwenye video kama ni Godfather, kama ni Adam, kama ni Moe Musa kama ni nani yeyote yule” Alisema Babu Tale kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top