Unknown Unknown Author
Title: Breaking News: Francis Cheka ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bondia mashuhuri nchini muda mfupi uliopita amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela. Hiyo ina maana kuwa Cheka anaenda kutumikia kifun...
Francis Cheka
Bondia mashuhuri nchini muda mfupi uliopita amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.Hiyo ina maana kuwa Cheka anaenda kutumikia kifungo hicho na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro.

Hukumu hiyo imetokana na kosa la bondia hiyo kumpiga meneja wake aitwaye Bahati kwenye bar ya Vijana Social mjini Morogoro July 2 mwaka jana alipoenda kudai fedha zake.

Meneja huyo alilazwa Hospitali kufuatia tukio hilo ambapo Cheka alidaiwa kumpiga ngumi. Katika kesi hiyo Cheka alikuwa anakana mashtaka.

Bondia huyo anaenda jela huku akiwa anashikilia mkanda wa dunia wa WBF Super Middleweight.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top