Unknown Unknown Author
Title: WALEMAVU WALIA NA MIUNDO MBINU ISIYO RAFIKI KWAO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Watu wenye ulemavu nchini wameiomba serikali na taasisi binafsi zinazotoa huduma za kijamii ikiwemo hospitali, benki na shule kuhakikisha k...
Watu wenye ulemavu nchini wameiomba serikali na taasisi binafsi zinazotoa huduma za kijamii ikiwemo hospitali, benki na shule kuhakikisha kuwa wanaweka miundombinu rafiki itakayowawezesha kuzifikia huduma hizo kwa urahisi.
Walemavu
Katibu wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu Arusha, Yunusi Urasa amesema kuwa kumekua na tatizo la la kukosekana kwa miundombinu rafiki kwa walemavu hali inayowakwamisha kupata huduma hizo muhimu kutokana na ulemavu walionao.

Yunusi aliyasema hayo jana katika semina ya watu wenye ulemavu iliyofanyika jijini Arusha na kuandaliwa na Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu nchini, ambapo amesema kuwa amehimiza serikali kuwakumbuka walemavu katika upangaji wa miji, ujenzi wa barabara na majengo ili waweze kupata haki zao za msingi za kunufaika na huduma za jamii.

Katibu huyo amependekeza kuwepo kwa dawati maalumu la kuwahudumia watu wenye mahitaji maalumu litakalowasaidia walemavu kupata huduma kwa urahisi.

“Mlemavu asiyeona akienda benki hawezi kutumia ATM card ni rahisi kuibiwa akikutana na mtu ambaye si mwaminifu, pegine zitengenezwe ambazo wataweza kuzisoma pia ATM ziko juu kwa walemavu wanaotambaa ni vigumu kuzifikia” Alisema Yunusi

Naye Katibu wa Chama cha Watu wenye ulemavu wa ngozi Arusha Happiness Raphael amesema kuwa wanashangazwa kuona mauaji ya albino yanaendelea huku mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa ya kikaa kimya hivyo ameiataka jamii ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha vitendo hivyo.

Mratibu wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini Francis Mhina amesema kuwa wanafanya juhudi za kutoa elimu kwa walemavu juu haki zao za msingi na namna ambayo wanaweza kujikwamua kimaisha, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni uhaba wa fedha hivyo kushindwa kuwafikia walemavu wengi ambao wako vijijini na kuishia mijini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top