Unknown Unknown Author
Title: #SPORTS MATOKEO YA MECHI ZA PREMIER LEAGUE JAN 10, 2014, CHELSEA. MAN CITY NA QPR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MENEJA mpya Alan Pardew ameanza vizuri huko Selhurts Park wakati Crystal Palace ilipotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitwanga Tottenham Bao 2...
Alan Pardew
MENEJA mpya Alan Pardew ameanza vizuri huko Selhurts Park wakati Crystal Palace ilipotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitwanga Tottenham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England.

Tottenham, ambao kwenye Mechi yao ya mwisho ya Ligi waliwashindilia Vinara wa Ligi Chelsea Bao 5-3, walitangulia kufunga kupitia Mchezaji wao anaeng’ara Harry Kane.

Palace walisawazisha kwa Penati ya Dwight Gayle iliyotolewa baada Benjamin Stambouli kumwangusha Joe Ledley na kisha kufunga Bao la ushindi kupitia Jason Puncheon.
Penati

Huo ni ushindi wa kwanza kwa Palace katika Mechi 8 na umewatoa toka kwenye zile Timu 3 za mkiani na kuwapandisha hadi Nafasi ya 15.

Ligi Kuu England inaendelea Leo kwa Mechi mbili kati ya Arsenal na Stoke City kisha Man United kucheza na Southampton.

VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni; Kelly, Delaney, Dann, Ward; Puncheon, Ledley, McArthur, Bannan; Gayle, Murray

Akiba: Hennessey, Mariappa, Guedioura, Hangeland, Thomas, Campbell, Zaha.

Tottenham Hotspur: Lloris; Walker, Fazio, Vertonghen, Rose; Dembele, Stambouli; Chadli, Eriksen, Townsend; Kane

Akiba: Vorm, Davies, Kaboul, Capoue, Lennon, Paulinho, Soldado.

Refa: Anthony Taylor

RATIBA: Saa za Bongo:: Jumapili Januari 11

1630 Arsenal v Stoke
1900 Man United v Southampton

Matokeo Mengine ya mechi za Premier League 10 Jan 2014, Liverpool, Chelsea, Man City na QPR
 
 
 
 
 
 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top