ALI KIBA ATANGAZA KUANZA MWAKA NA "SURPRISE"

Star wa muziki Ali Kiba, amesema kuwa mapokezi ya video yake ya Mwana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania yamekuwa ni ishara kwake kuwa kuna mtu alikuwa amemiss katika game na katika mchango wa kuitangaza nchi kimataifa kupitia sanaa.
ALI KIBA
Ali Kiba akiwa katika ofisi za EATV alipofanya ziara maalum siku ya Jumamosi Tarehe 09/01/2015

Kiba ameiambia eNewz kuwa amefurahi kuona mashabiki wamempokea tena vizuri na kumpa nguvu ya kuendelea kuwatengenezea kazi zenye viwango vya kimataifa.
Kuhusiana na kiu ya mashabiki wengi kujua Kiba mwaka huu ana uanzaje, na vilevile kuhusiana na kolabo za kimataifa, Kiba amesema mipango imeshasukwa, akiwa amejipanga kutoa kazi kwa mtindo wa Bumper 2 Bumper, mpango utakaoanza mwezi huu wa Januari.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post