Unknown Unknown Author
Title: OMMY DIMPOZ NA DIAMOND KUONESHANA MAKALI KATIKA TUZO ZA HMA - UGANDA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ommy Dimpoz na Diamond wakipeana mkono wa kheri  Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platinum na Ommy Dimpoz wamet...
Ommy Dimpoz na Diamond
Ommy Dimpoz na Diamond wakipeana mkono wa kheri 

Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platinum na Ommy Dimpoz wametajwa kuwania tuzo za muziki za nchini Uganda ziitwazo HiPipo Music Awards (HMA) 2015 zinazotarajiwa kutolewa rasmi February 07, 2015.

Diamond na Dimpoz watachuana katika kipengele kimoja cha ‘East Africa Super Hit’ kupitia nyimbo zao Ndagushima na Number One original.

Katika kipengele hicho wakali hao watachuana na Sauti Sol, Jaguar, Eddy Kenzo, Baramushaka, Urban Boys na Bebe Cool.

Aidha, hatua hiyo inaonesha jinsi muziki wa Bongo flava unavyoendelea kufanya vizuri katika soko la muziki la kimataifa na jinsi unavyokubalika kwa kasi kubwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top