Unknown Unknown Author
Title: LIVERPOOL YAPATA SARE DHIDI YA ARSENAL, GOLI LA LALASALAMA LA MARTINI SKERTEL
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Goli la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Martin Skrtel (pichani) dakika saba ndani ya muda wa nyongeza leo umewapa Liverpool ushindi ...
Goli la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Martin Skrtel (pichani) dakika saba ndani ya muda wa nyongeza leo umewapa Liverpool ushindi waliostahili dhidi ya Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield.
Refa Michael Oliver aliongeza dakika tisa kufuatia mpira kusimama kwa muda mrefu baada ya Skrtel kuumizwa na kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kugongana kwa bahati mbaya na Olivier Giroud wa Arsenal.

Giroud alionekana tayari kaipaisha Arsenal kuelekea kwenye kulipiza kisasi cha kupigwa bao 5-1 hapo hapo Anfield msimu uliopita baada ya kufunga bao la kuongoza, baada ya Mathieu Debuchy kusawazisha sekunde chache kufuatia bao la Liverpool la kuongoza lililofungwa na Philippe Coutinho dakika moja kabla ya mapumziko. 

Lakini Skrtel, akiwa amefungwa bandeji kubwa kichwani huku Liverpool wakiwa watu 10 kufuatia mchezaji wa akiba Fabio Borini kutolewa nje kwa mchezo mbaya, alipaa hewani na kuweka kimiani mpira wa kona uliopigwa na Adam Lallan dakika ya 97 na kumpita kipa Wojciech Szczesny mbele ya mashabiki maarufu wa Bwawa la Maini - The Kop.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top