Unknown Unknown Author
Title: ZOEZI LA MAOMBI YA PASIPOTI KWA WATANZANIA NCHINI ITALI LAENDELEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Afisa Uhamiaji akichukua maelezo ya mmoja wa Watanzania waishio nchini Italy wakati wa zoezi la kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzani...
Afisa Uhamiaji akichukua maelezo ya mmoja wa Watanzania waishio nchini Italy wakati wa zoezi la kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania hao.
Baadhi ya Maofisa wa Uhamiaji ambao wako nchini Italy hivi sasa,wakiendelea na kazi rasmi ya kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania waishio nchini humo, wakiwa katika siku ya pili ya zoezi hilo,ambalo linaanzia asubuhi mapema saa 3 hadi saa kumi na mbili jioni.
Sehemu ya Watanzania hao wakisubiri kutatuliwa matatizo yao ya pasipoti.

Na. Mwandishi Wetu


Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania waliopo nchini Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea katika nchi za Turkey na Greece,kwa ajili ya zoezi hilo hilo.

Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora iliyokutana na Mh Balozi James Alex Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy .
Mkutano huo uliisha kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh Balozi Dkt James Alex Msekela, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August mwaka huu alitumia muda wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top