Unknown Unknown Author
Title: MARKET FC YAIBANJUA KARIAKOO FC YA YUSUF MACHO 1 - 0
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bechi la Ufundi la Timu ya Market Fc katika mechi dhidi ya Kariakoo Fc Ndani ya Uwanja wa Ilulu, 2/10/2014. Bechi la Ufundi la Timu...
market fc vs Kariakoo fc
Bechi la Ufundi la Timu ya Market Fc katika mechi dhidi ya Kariakoo Fc Ndani ya Uwanja wa Ilulu, 2/10/2014.
market fc vs Kariakoo fc

Bechi la Ufundi la Timu ya Kariakoo Fc katika mechi dhidi ya Market Fc Ndani ya Uwanja wa Ilulu, 2/10/2014.

Na. Mwandishi Wetu
Timu inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Soko Kuu Mkoa wa Lindi Market Fc, imeibuka kidedea katika Mchezo wake wa kwanza wa kirafiki uliochezwa hapo jana dhidi ya Timu Kongwe ya Mjini Hapa ya Timu ya Kariakoo kwa kuifunga Goli Moja kwa bila.

Awali Mchezo huo wa kirafiki ulitakiwa kuzikutanisha Timu za Kariakoo Fc ya Mjini Lindi na Azam Fc ya Dar es salaam lakini ukaahirishwa na kufanya waandaaji wa mechi hiyo kuwapa nafasi timu hiyo ya Market Fc ya Mkoani hapa kucheza Dhidi ya Kariakoo Fc.
market fc vs Kariakoo fc

Timu hizo zikiwa zinajiandaa na mashindano tofauti zilipimana nguvu ndani ya Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi, Huku Timu zote zikiwa zinakutana mara ya kwanza kwa Mwaka huu huku wakiwa na vikosi vipya kabisa vya ushindani.

Mchezo Huo ulianza majira ya Saa kumi na Nusu Jioni, Timu hizo zilicheza kwa kuviziana katika kipindi chote cha Kwanza na kufanya matokeo kubakia 0 -0 hadi kipenga cha Mapunzika kilivyopulizwa.
market fc vs Kariakoo fc
Kipindi Chapili kilianza kwa kasi kwa Timu zote mbili kutaka kumfunga mpinzani wake lakini Beki zote zilionekana kuwa vizuri san kwa kuto ruhusu mashambulizi langoni mwao. Lakini Timu ya Market Fc ilionekana kuwamudu Kariakoo Fc kuanzia dakika ya 60 ya mchezo katika kipindi hicho cha pili.

Heka heka hizo zilizaa matunda mnamo dakika ya 72 kupitia mchezaji wake Hemed Mbela Kuipatia Goli la Kwanza timu yake ya Market Fc na Kuwa goli la Ushindi katika Mchezo huo.
market fc vs Kariakoo fc
Viongozi wa Timu ya Market Fc walijigamba mwisho wa Mchezo huo kwa Kusema kwa sasa wako vizuri na wanaendelea na mazoezi ya kuijega timu yao hiyo ili ije kuwa mwiba katika mashindano ya Usoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top