Unknown Unknown Author
Title: PRODUCER WA "MY NUMBER 1" YA DIAMOND PLATNUMZ SASA AVUKA BODA, ATAYARISHA NYIMBO ZA TIWA SAVAGE NA KCEE WA NIGERIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Producer wa hit single ya Diamond Platnumz, Number One , Sheddy Clever ametayarisha nyimbo za wasanii wakubwa wa Nigeria, Tiwa Savage na ...
Producer wa hit single ya Diamond Platnumz, Number One, Sheddy Clever ametayarisha nyimbo za wasanii wakubwa wa Nigeria, Tiwa Savage na KCEE.
Sheddy ambaye ana studio yake iitwayo Burn Records, amesema kuwa fursa ya kutayarisha nyimbo za wasanii hao imepatikana kutokana na connection aliyofanyiwa na Diamond. “Tayari nimeshafanya kazi na Tiwa Savage na kuna kazi ambayo nimefanya na KCEE na kuwa wasanii wengine wa South Africa,” amesema Sheddy ambaye alitajwa kuwania kipengele cha mtayarishaji bora wa muziki wa Afrika kwenye tuzo za AFRIMMA 2014.

“Zote ni connection za Diamond, yeye (Tiwa Savage) anafahamiana naye na mimi nilimwambia Diamond ‘nahitaji kufanya naye kazi’ Diamond akaniambia ‘Yeah it’s okay, fanya beat’ akaniunganisha naye, nikawa nachat naye, nikamtumia beat akapenda, tukawa tunafanya kazi online, na ana ngoma pia amefanya na Diamond.”

“Amesharekodi tayari kila kitu na wimbo upo, kwahiyo sasa ni yeye tu sijui atatoa lini ila mimi nahitaji project hizo mwakani ntaomba ruhusa kutoka kwao ili niziachie hapa nyumbani,” aliongeza Sheddy.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top