Unknown Unknown Author
Title: CHADEMA NACHINGWEA WAMTETEA WARIOBA, WATAKA ASISAKAMWE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wilaya Nachingwea mkoa wa Lindi, kimetoa wito kwa wote wanomlaumu na kumshambulia aliyekuwa Mwe...
Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) wilaya Nachingwea mkoa wa Lindi, kimetoa wito kwa wote wanomlaumu na kumshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya kukusanya maoni ya Katiba, Jaji Joseph Warioba waache kufanya hivyo.
Lindiyetu News

Wito huo ulitolewa jana mjini Nachingwea na katibu wa wilaya wa chama hicho,Yassin Nakanyomwa alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari. Nakanyomwa alisema kuendelea na mkushambulia Jaji Warioba ni dalili inayoonesha kuwa ustaarabu miongoni mwa waTanzania unatoweka kwa kasi.Kwa madai kwamba mzee huyo ni miongoni mwa watu wachache ambao wanania njema kwa maendeleo na ustawi wa nchi hii.
Jaji Warioba
Alisema kuendelea kumsakama kwa jambo ambalo lilikuwa niwajibu wake kulifanya baada ya kutumwa ni kutomtendea haki na nidhambi "Jaji Warioba amekosea nini kwani yaliyokuwa kwenye rasimu yalikuwa ni maoni ya wananchi, matusi anayotukanwa ni ushaidi kuwa sifa ya ustaarabu tuliyokuwa nayo inatoweka kwa kasi kubwa," alisema Nakanyomwa.

Katibu huyo aliongeza kusema watu wanaofanya hivyo wasione kama wanamshambulia Warioba peke yake bali hata aliyemteua kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo na wananchi kwa madai kuwa hajajipa nafasi hiyo na maoni hayakuwa yake. Aidha alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa watulivu na wamoja baada ya bunge la katiba kupitisha rasimu ya katiba kwani itafikishwa kwa wananchi ili waipigie kura.
"Hakuna haja ya kugombana tume ilitimiza wajibu wake na bunge la katiba limetimiza wajibu wake bado sisi wananchi watakapotuletea hiyo rasimu tutafanya uamuzi ndipo mbichi ma mbivu zitajulikana," aliasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top