Unknown Unknown Author
Title: JIPYA KUHUSU UHAMISHO WA KUDUMU WA FALCAO MANCHESTER UNITED
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati mkataba wake wa mkopo ukiwa umebakisha miezi nane kuisha, usajili wa Radamel Falcao kwenda Manchester United umechukua nafasi kwenye...
Wakati mkataba wake wa mkopo ukiwa umebakisha miezi nane kuisha, usajili wa Radamel Falcao kwenda Manchester United umechukua nafasi kwenye vyombo vya habari vya Uingereza vinavyoripoti kwamba Man United imekubaliana rasmi na mahitaji binafsi ya mchezaji huyo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kudumu.
Falcao
Taarifa zinaeleza kwamba Man United wanafanya jitihada zote kumaliza suala la usajili wa Falcao ili kuepuka kila kilichotokea miaka mitano iliyopita katika usajili wa Carlos Tevez……. United walimsajili Falcao kwa mkopo kutoka Monaco siku ya mwisho ya usajili wa wakati wa kiangazi.

Wakiwa tayari wameshalipa ada ya mkopo wa £6million kwa klabu ya Ufaransa, United pia walishakubaliana kimsingi na Monaco kuwalipa kiasi cha £43.5m ikiwa wataamua kumchukua Falcao kiujumla mwishoni mwa msimu.

Baada ya hayo yote, leo imeripotiwa kwamba mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward tayari amekubaliana na wawakilishi wa Falcao kumlipa mshahara wa £250,000 kwa wiki mchezaji huyo pamoja na bonasi na haki za taswira yake kutumika ambapo kwenye sentensi nyingine club hii imekanusha taarifa kwamba itakatisha mkataba wa mkopo wa Falcao ikiwa mchezaji huyo ataumia tena goti.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top