Unknown Unknown Author
Title: BIRTHDAY PARTY YA DIAMOND PLATNUMZ IMEELEZWA KUGHALIMU TSH M28, ZAWADI YA GARI NI TSH M90
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platnumz ni msanii ambaye yuko kwenye level za juu kwenye kila kitu kwa sasa, upande wa muziki na hata aina ya maisha anayoishi. Hi...
Diamond Platnumz ni msanii ambaye yuko kwenye level za juu kwenye kila kitu kwa sasa, upande wa muziki na hata aina ya maisha anayoishi. Hilo linaweza kuthibitishwa na gharama zilizotumika kufanikisha sherehe yake ya kutimiza miaka 25 iliyofanyika jana October 2, pamoja na zawadi aliyopewa na uongozi wake.
Diamond Platnumz
Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema party hiyo iligharimu shilingi milioni 28 na kuwataja waliohusika kuigharamia.

“Event tumefanya wenyewe lakini mwisho wa siku Diamond yupo karibu na watu wengi na makampuni mengi”
Tale ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “Coca cola kama Coca Cola ndio walichukua nafasi kubwa kuifanya ile event sababu wao ni balozi wao….ilikuwa gharama inagharimu milioni 28 kwa sisi wenyewe watoto wa paka tusingeweza kuitoa kirahisi hiyo hela.”

Zawadi kubwa aliyopata Diamond kwenye birthday yake ni gari aina ya BMW X6, ambayo alipewa na uongozi wake unaoundwa na Babu Tale, Said Fela na Salam. Tale ameelezea jinsi walivyoweza kupata pesa za kununua gari hiyo.

“Sasa hivi Diamond anafanya vizuri na tulikuwa tunamwambia Diamond kwamba kuna contract tukisaini tutakupa zawadi, as in kwamba management haitachukua percent ya hiyo contract hiyo pesa itaenda kwenye kukuchukulia wewe zawadi, akasema nyie bana mlivyokuwa watata sijui kama mtakubali.”

Aliendelea,“Tulivyotoka South Africa tukawa kuna contract tume confirm kusaini, tulivyosaini ile contract ile pesa ambayo ilitakiwa pasenti yote ije kwetu sisi mimi, Fela na Salam yote tukasema tumchukulie zawadi….ni shilingi ya kitanzania milioni 90”.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top