Unknown Unknown Author
Title: BREAKING NEWS: MSANII CHID BENZ AKAMATWA NA POLISI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Najua kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoan...
Najua kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid Benz amekamatwa na Polisi.
Chidi benzi
Taarifa zinasema kakamatwa na Polisi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Mbeya na hiyo imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni kosa kwa yeyote kukutwa navyo.

Wakati millardayo.com inaendelea kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi, tumezungumza na muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz ndio alikua anakwenda kushiriki kesho.

Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu  “Sijapewa taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba haviruhusiwi kupita Airport".

Chidi Benz alikua ameongozana na msanii mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi kabaki na Polisi na Shetta amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea Mbeya.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top