AFYA:: MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA NI KINGA YA UGONJWA WA KUPOOZA.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Moyo Marekani (American Heart Association) unaonyesha kuwa mboga za majani na matunda ni kinga sahihi ya kumwondoa binadamu kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza.
MATUNDA 
Utafiti huo umekuja baada ya kubainika kuwa ugonjwa wa kupooza umezidi kushika kasi hasa kwa mataifa ambayo yana watu wenye vipato vikubwa.

Wataalamu walioshiriki katika utafiti huo walieleza kuwa vitamin zilizopo kwenye matunda na mboga za majani zina uwezo mkubwa wa kumwondoa mlaji kwenye hatari ya kupooza.

“Inaweza kuonekana ni kitu cha ajabu lakini ndiyo ukweli ulaji wa matunda na mboga za majani ni kinga ya asili ambayo inaweza kumwondoa binadamu katika hatari ya kupooza,” alisema Dk John Baden.

Utafiti huo unaenda sanjari na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo inaeleza kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huo kwa asilimia 19.

Nchini China ugonjwa wa kupooza unatajwa kusababisha vifo vya watu wengi kuliko magonjwa mengine.
********************************************
LindiYetu.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani, Siasa, Michezo ya Africa na Nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram Twitter Na Facebook

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post