Unknown Unknown Author
Title: SOMA HII KWA UMAKINI "SIYO KILA JAMBO NI LA KUULIZA"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Usimuulize yatima: Babako alikufa vipi au mamako alikufaje? Na usiwaulize wazazi: Mtoto wenu alikufaje? Na usimuulize mtu asiye na kazi, ...
siyo kila jambo ni la kuuliza
Usimuulize yatima:
Babako alikufa vipi au mamako alikufaje?
Na usiwaulize wazazi:
Mtoto wenu alikufaje?
Na usimuulize mtu asiye na kazi, mbele za watu:
Wewe kwanini hufanyi kazi?
Usimcheke mwenye watoto mabadhuli 
Hujuwi wakakwo watakuaje
Na usimuulize maskini:
Wataka pesa? Mpe bila ya kumuuliza, hivi ni kumkirimu khasa akiwa ataonana nawe mara kwa mara.
Na usimuulize mwanamke asiyezaa:
Wewe huna watoto?
Na usimuulize ambaye ana alama usoni sababu yake! 
Kwani uso ni sehemu ya utukufu.
Na usimcheke kilema 
Kwani hakuomba kumbuka hujafa hujaumbika
Na usimuulize mgeni:
Unataka chakula? Au kinywaji? Mpe bila ya kumuuliza, ukimuuliza unamnyima.
Na usimuulize mwanamwali 
Sababu ya kuchelewa kuolewa.
Wala Usimuilize mwanamke 
Kwanini umekubali kuolewa ktk ukewenza asije mmeo akaoa kesho
Usije ukamuuliza mtu kwanini Mumeo anazaidi ya mmoja
Na usijaribu kumfanyia stihzai rafiki kwa ajili ya kutaka kufurahisha wengine..
kwani inamuumiza sana!
Daima jiweke mahala pa mpokezi na ujaribu kuhisi hisia zake♡ !
"Mkono kwa mkono hadi peponi" 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top