Unknown Unknown Author
Title: MAJAMBAZI WANAOHUSISHWA NA MAUAJI YA SISTA WA KANISA KATOLIKI WASHIKILIWA NA POLISI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu nane wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi sugu. Wawili kati yao wan...
JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu nane wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi sugu. Wawili kati yao wanahusishwa na tukio la kuuawa kwa Sista Cresencia Kapuri (50) wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Parokia ya Makoka.
lindiyetu news
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jana.

Alisema wahutuhumiwa hao, wakiwa katika utekelezaji wa uhalifu wao, walisababisha vifo, majeraha, wizi wa mali na fedha taslimu.

Alisema watuhumiwa hao, walitumia silaha za moto, ikiwa ni pamoja na bunduki aina ya SMG, bastola na vifaa mbalimbali vya uvunjaji, ikiwa ni pamoja na baruti.

Alitaja watuhumiwa wanaohusishwa na tukio la kuuawa kwa Sista Cresencia kuwa ni Manase Ogenyeka (35), maarufu kama Mjeshi, mkazi wa Tabata Chang’ombe Manispaa ya Ilala, ambaye ni dereva wa bodaboda ; na Hamisi Shaaban maarufu kama Carlos, mfanyabiashara, mkazi wa Magomeni Mwembechai Manispaa ya Kinondoni.
Sista huyo aliyekuwa pia Mhasibu wa Parokia ya Makoka na Mhasibu wa Shule ya Mwenyeheri Anwarite inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, aliuawa kwa kupigwa risasi Juni 23, mwaka huu katika eneo la Riverside, Ubungo Kibangu, Dar es Salaam. Kova alisema licha ya kuhusishwa na kifo cha Sista huyo, watu hao wanatuhumiwa kupora Sh milioni 20.

Alisema watuhumiwa hao, pia walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uporaji wa Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni, uliotokea Aprili 28, mwaka huu, ambapo mamilioni ya fedha yaliibwa kabla na baada ya tukio hilo.

“Jambazi Manase Ogenyeka ndiye aliyeendesha pikipiki, akimbeba mwenzake akiwa na fuko la mamilioni ya fedha na kutoroka nazo wakati Hamisi Shaaban ndiye aliyekuwa kiongozi katika tukio hilo,” alidai Kova.

Mbali ya kuuawa kwa Sista Cresencia, katika tukio hilo aliongozana na Sista Brigita Mbaga (32) na dereva wao, Mark Mwarabu, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux Pick-Up, lenye namba T213 CJZ ambaye alikatwa dole gumba lake kwa risasi baada ya kushambuliwa.

Alisema Jeshi la Polisi, bado linawatafuta watuhumiwa wengine wawili katika tukio la kuuawa kwa Sista. Mtu mwingine anayetafutwa ni Leonard Molel anayetuhimwa kwa tukio la wizi katika Benki ya Barclays.

Kamanda huyo alisema watuhumiwa wengine watatu, kati ya hao wanane, walikamatwa baada ya kutumia mbinu ya hati bandia wakiwa wanaomba kazi katika kampuni binafsi ya ulinzi iitwayo Instant Security Services Mtaa wa Makangira Msasani, Dar es Salaam.

Hao ni Elibariki Makumba (30) na Nurdin Suleimani (40), wakazi wa Buguruni Madenge na Mrumi Salehe(38), mkazi wa Kigogo Fresh.

Alitoa rai kwa kampuni za ulinzi, yanapotaka kuajiri walishirikishe Jeshi la Polisi ili wafanye upekuzi wa pamoja, utakaohusisha alama za vidole, picha na ukaguzi wa kumbukumbu muhimu za kibayolojia kama vile vipimo vya DNA.

Aidha, aliwaomba wananchi ambao wana tabia ya kutembea na fedha nyingi, kuacha kufanya hivyo, kwani kwa sasa teknolojia imepanuka, hivyo kuweza kutumia simu za mkononi kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top