Bao la Mexico lilifungwa na Straika wa Villareal Giovani Dos Santos katika Dakika ya 48 kwa Shuti kali la chini.
Netherlands walisawazisha Dakika ya 88 baada Wesley Sneijder kuunasa Mpira ndani ya Boksi na kufumua shuti.

Katika Dakika za Nyongeza baada ya Dakika 90 kumalizika, Arjen Robben alitumbukia ndani ya Boksi na kuanza kutambuka Mabeki lakini akaja Beki Mkongwe Rafael Marquez na kumwangusha na Refa Pedro Proenca akaashiria Penati na kumpa Beki huyo wa Mexico Kadi ya Njano.

Penati hiyo ilifungwa na Klaas-Jan Huntelaar, alieingizwa mwishoni Kipindi cha Pili kuchukua nafasi ya Nahodha Robin van Persie, katika Dakika ya 94 na kuifanya Netherlands waongoze 2-1 na hatimae kushinda kwa Bao hizo.

Kwenye Mechi hii, kutokana na Joto kali ambalo lilifikia Digrii 39C, FIFA iliruhusu Mechi kusimamishwa na Refa kutoka Portugal, Pedro Proenca, mara mbili kwa Dakika 3 kila wakati ili Wachezaji kujipoza kwa kunywa Maji, kujimwagia Maji na kujifunika Vitambaa vya Maji.
Mapumziko hayo yalikuwa kwenye Dakika ya 32 ya Kipindi cha Kwanza na Dakika ya 77 ya Kipindi cha Pili.
Dakika hizo 3 ziliongezwa mwishoni mwa kila Kipindi.
Netherlands sasa wametinga Robo Fainali na watacheza na Mshindi kati ya Costa Rica na Greece wanaocheza baadae Leo hii.
VIKOSI: Holland: Cillessen, Verhaegh, Kuyt, Vlaar, De Vrij, Blind, De Jong, Wijnaldum, Sneijder. Van Persie, Robben
Akiba: Vorm, Krul, Martins Indi, Janmaat, De Guzman, Veltman, Kongolo, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Memphis.
Mexico: Ochoa, RodrÃguez, Salcido, Márquez, Herrera, Layún, Dos Santos, Moreno, Guardado, Peralta, Aguilar
Akiba: Corona, Talavera, Reyes, Fabián, Jiménez, Pulido, Hernández, Ponce, Brizuela, Aquino, Peña, Vázquez.
Refa: Pedro Proença (Portugal)

Tags
SPORTS NEWS