Unknown Unknown Author
Title: MASHINDANO YA SAFARI LAGER POOL TABLE CHAMPIONSHIP YAMALIZIKA MKOANI LINDI, NA BLUELEAF KUIBUKA KIDEDEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Blue leaf Bar wakishangilia Ushindi huku wakiwa na Zawadi yao ya Mshindi wa Kwanza kitita cha Tsh 800,000/= Mashindano ya Sa...
safari lager pool championship
Timu ya Blue leaf Bar wakishangilia Ushindi huku wakiwa na Zawadi yao ya Mshindi wa Kwanza kitita cha Tsh 800,000/=

Mashindano ya Safari Lager Championship yamemalizika hapo jana Mkoani Lindi kwa kupata washindi mbalimbali wa mchezo huo ambao washindi hao wataweza kuuwakilisha Mkoa wa Lindi katika Mashindano hayo Kitaifa Mjini Moshi Mwezi wa Kumi mwaka huu.
safari lager pool championship
Mgeni Rasmi wa Mashindano hayo (katikati) Saida Mponjoli akiwa na Refa wa Mashindano hayo (wakushoto) Shabani Mponda

Akiongea mara baada ya Mashindano hayo kumalizika Afisa Vijana wa Mkoa wa Lindi Dada Saida Mponjoli amesema kuwa Anawashukuru sana Vijana hao kwa kujitokeza kushiriki mashindano hayo kwani mashindano hudumusha amani na pia huongeza maarifa kwa kujifunza vitumbalimbali, aidha amewataka kuitumia fursa hiyo kuiwakilisha vizuri mkoa wa Lindi katika Mashindano ya Kitaifa yatakayofanyika Mjini Moshi na kuwaambia kuwa wanaweza kuwa wamoja kati ya wale watakaoweza kuchaguliwa kuunda timu ya Taifa ambayo itashiriki Mchezo huo na nchini Nyingine za Nje hivyo waongeze Juhudi.

Zawadi zilitolewa kwa Mshiriki Moja moja na Kwa Kiteaam. 
safari lager pool championship
Kutoka Kushoto:: Mshindi 4 , 3 , 2, 1

Mshiriki Moja moja (Single Player) Kwa Upande wa wanawake, Mshindi wa Nne aliweza Kujinyakulia Kitita cha Shilingi 50,000/= , Mshindi wa tatu aliweza Pata Tsh 100,000/= , Mshindi wa Pili aliweza Kujinyakulia Tsh 200,000/= Na Mshindi wa Kwanza aliweza kupata Kitita cha Tsh 300,000/=
Kutoka Kushoto: Mshindi wa 1,2,3 na 4

Washindi wa Kiume kwa Mshiriki Mmoja mmoja (Single Player) Namba nne alipata kitita cha Tsh 100,000/= , Na Mshindi wa Tatu alipata kiasi cha Tsh 150,000/= , wa pili alinyakua kitita cha Tsh 200,000/= na Mshindi wa Kwanza alipata zawadi ya Kiasi cha Tsh 400,000/=.
safari lager pool championship
Katika Zawadi za makundi (Team) Mshindi wa Nne alipata Tsh 150,000/= ambaye ni Santolini Pool Club, Mshindi wa tatu alipata Kiasi cha Tsh 200,000/= ambaye ni Fisi Pool Club, Mshindi wa Pili ambaye ndio mwenyeji wa mashindano hayo Bwalo Pool Club aliibuka na Kitita cha Tsh 400,000/= Huku Mshindi wa Kwanza ambaye hii ni mara yake ya kwanza kushiriki katika mashindano hayo Blue Leaf Pool Club iliweza kuibuka kidedea na Kunyakua kitita cha Tsh 800,000/=.

Mshindano hayo yalikuwa ya kuvutia sana Hasa katika Mechi ya Mwisho wa kumtafuta bingwa wa Mkoa kwani washiriki walikuwa wanafungana zamu kwa zamu. Team ya Blue Leaf Ndio ya kwanza kuifunga Timu ya Bwalo la Polis kwa Michezo 11 - 5, na kubakiwa na michezo miwili tu kumaliza mchezo na kuibuka bingwa lakini vijana wa Timu ya Bwalo la Polisi walizinduka na Kuweza Kuwasimamisha Blue Leaf .
Kijana Pembe Saidi Kuiwezesha timu yake ya Blue leaf Kuwa Bingwa wa Safari Lager Champions 2014 wa Mkoa wa Lindi kwa Kumaliza Game ya 13 -11.

Hizi ni Baadhi ya Picha za Matukio hayo. 
safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

 safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

safari lager pool championship

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top