Na. Zakayo Nkwera
Habari zenu wadau, natumai mmeamka mkiwa wazima wa Afya na kama kuna mmoja wetu anae umwa au anatatizo lolote lile basi kwapamoja tumuombe Mungu atuonyeshe mlango wa kutokea ili tuendelee kuwa na furaha. Leo ni siku nyingine ningependa tuongelee mada ya wajibu wa Baba na Mama katika kumlea mtoto:
Mtoto hatokei kama mzimu bali wazazi wanamtafuta na Mungu akijalia wanampata wenye tunawaita matunda ya upendo katika familia.
Tatizo linakuja nani mwenye jukumu la kumlea na kuanzia wakati gani?Wote wawili wanalo jukumu, na tangu ujauzito ulipotunga wazazi wote wanapaswa kuanza kumlea kwa pamoja.Ujauzito tutautunzaje wote wawili?Mwanaume kwa kuonyesha upendo kwa mkeo kwa kumsaidia kazi, kumpa huduma anazostahili kwa kipindi hicho.
Nani anapaswa kwenda kliniki kupima ujauzito?Hapo ndio kunatatizo, wote wawili mume na mke tunapaswa kwenda klini kupima mkeo atapimwa ujauzito ila wote mtapimwa magonjwa ili kuilinda afya ya mtoto na yenu pia na wote mtapewa ushauri ni jinsi gani mnatakiwa kumlea vizuri mtoto wenu akiwa tumboni na hata akizaliwa.Kwanini twende wote? jibu ni kwasababu ni mtoto wetu wote.Faida ni zipi tukienda wote?
- Mtajua afya zenu
- kama mmeathilika mtafundishwa jinsi ya kumpata mtoto asiye na virusi
- Utapewa mbinu za kujiandaa kiuchumi kwaajili ya kumpokea mwanao
- Hospital nyingi kama sio zote hutoa vipaumbele kwa wale walioenda klini na waume zao au waume walionda peke yao na watoto kliniki
- Na ya mwisho ingawa ndio ya kwanza kwa umuhimu ni upendo utakuwa umejenga upendo mkubwa sana kwa mkeo na mtoto wako.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.