VIDEO MPYA YA WIMBO WA KOMBE LA DUNIA YA SHAKIRA, HII HAPA MESSI,NEYMAR NA WENGINE NDANI

Shakira - La La La (Dare)
Nadhani wote mnakumbuka ule wimbo maalum kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 wa ‘wakawaka’ ulioimbwa na Shakira ambapo this time kwenye kombe la dunia baada ya ule kufanya vizuri… mwaka huu Shakira amepata shavu jingine la kufanya wimbo wa kombe la dunia litakalofanyika Brazil kuanzia mwezi ujao.
Shakira - La La La (Dare)Wimbo huo umepewa jina la La La La (Dare) na video yake tayari imetoka na ndani yake imehusisha familia nzima ya Shakira, mwanae pamoja na mpenzi wake ambaye ni mwanasoka wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Spain Gerard Pique.

Wachezaji wengine walionekana kwenye video hiyo ni Lionel Messi, Aguero, Radamel Falcao na wengine wengi. Hadi sasa Video hiyo imetazamwa na watazamaji zaidi ya Laki Tano Tangu iwekwe You tube Leo hii, itazame hapa chini…

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post