United wamekubaliana na Bayern Munich kuuziana Toni Kroos
Kross alikubaliana na ofa ya paundi milioni 20 na aliyekuwa kocha wa Manchester United, David Moyes na mrithi wake ambaye aliyewahi kuwa kocha wa Bayern Munich, Louis Van Gaal amebariki dili hilo kuendelea.

Yupo kwenye rada: United kwasasa wapo katika mawindo ya kumnasa nyota wa Bayern, Arjen Robben

Tabasamu tu: Kocha wa Uholanzi, Louis Van Gaal akitasamu katika mazoezi ya timu yake mjini Lagos nchini Ureno.
Siku za karibuni winga huyo mwenye miaka 20 alisaini mkataba wa miaka mitatu na Bayern, lakini haimvunji moyo Van Gaal ambaye atafanya kazi na Robben katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Inafahamika kuwa United wamekubaliana dili la paundi milioni 27 ili kuinasa saini ya beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw na beki wa kati wa Borussia Dortmund, Mats Hummels yupo katika mipango ya Van Gaal.
Tags
SPORTS NEWS
