Unknown Unknown Author
Title: MAN CITY WAFYATA MKIA KWA YAYA TOURE, SASA KUFANYA MAZUNGUMZO YA AMANI KUEPUSHA SHARI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jembe la kazi: Yaya Toure ametikisa kiberiti Man City kwa kudai anataka kuondoka baada ya klabu yake kushindwa kuthamini siku yake ya kuz...
Yaya Toure
Jembe la kazi: Yaya Toure ametikisa kiberiti Man City kwa kudai anataka kuondoka baada ya klabu yake kushindwa kuthamini siku yake ya kuzaliwa.

MANCHESTER City yasalimu amri kwa mwafrika Yaya Toure baada ya mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo, Txiki Begiristain kusema atakuwa na mazungumzo ya amani na kiungo huyo kwa lengo la kumaliza tofauti zao zilizojitokeza siku za karibuni.Wakala wa Toure, Dimitry Seluk aliibua shari jumanne ya wiki hii kwa kusema kuwa kiungo huyo anaweza kuihama Man city majira ya kiangazi mwaka huu kutokana na mabingwa hao wapya wa ligi kuu England na mmliki wake Sheik Mansour kushindwa kuithamini siku yake ya kuzaliwa wakiwa katika ziara ya baada ya msimu mjini Abu Dhabi wiki iliyopita.

Kuna taarifa kuwa Seluk anataka kumrejesha Yaya katika klabu ya Barcelona ambako alihama mwaka 2010 kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 24 na sasa ni moja ya wachezaji bora kabisa wanaotegemewa na Man City.

Dimitri Seluk
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk aliibua shari kwa kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota huyo kuondoka Etihad
Yaya Toure
Tabasamu: Toure kwasasa yupo katika kambi ya timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya ziara ya baada ya msimu mjini Abu Dhabi na klabu yake ya Man City.

Toure amefunga mabao 24 katika mechi 49 alizoichezea Man City msimu uliopita na kukiwezesha kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kutwaa ubingwa.

City wameshikilia msimamo wao kuwa Toure hataondoka kwasababu bado ana miaka mitatu katika mkataba wake aliosaini miezi 12 iliyopita na unampatia paundi laki mbili kwa wiki.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top