Unknown Unknown Author
Title: SCOLARI AKUMBWA NA KASHFA YA KUKWEPA KULIPA KODI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ikiwa ni siku chache pekee zimebaki kwa mashindano ya kombe la dunia yaanze kutimua vumbi nchini Brazil,kocha wa timu ya taifa hilo Luiz ...
Luiz Felipe Scolari
Ikiwa ni siku chache pekee zimebaki kwa mashindano ya kombe la dunia yaanze kutimua vumbi nchini Brazil,kocha wa timu ya taifa hilo Luiz Felipe Scolari anachunguzwa kwa kosa la kukwepa kodi nchini Ureno.

Gazeti la michezo nchini Brazil Folha de S.Paulo limesema kocha huyo anachunguzwa na serikali ya Ureno kwa deni hilo la kodi linalofikia €7m(5.7m).

Hii ni kati ya mwaka 2003-2008 wakati Scolari akiwa kocha wa timu ya taifa hilo.
Hata hivyo Scolari amejibu mapigo kwa kusema hakuwahi kufanya kosa hilo Ureno na sehemu nyingine alizowahi kufanya kazi.
Ameongeza kama kuna makosa yamefanyika hivyo siyo kosa lake bali ni la mamlaka inayohusika ila yeye alilipa na hakukwepa kodi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top