Unknown Unknown Author
Title: MUTHARIKA RAIS MPYA MALAWI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mgombea wa Chama cha upinzani nchini Malawi Peter Mutharika ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais uliozua utata. Mutharika wa Cham...
Mutharika
Mgombea wa Chama cha upinzani nchini Malawi Peter Mutharika ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais uliozua utata.

Mutharika wa Chama cha Democratic Progressive Party amepata asilimia 36.4 ya kura, imetangaza tume ya uchaguzi nchini humo.

Rais anayeondoka madarakani Joyce Banda amedai uchaguzi huo ulivurugwa.
Tume ya uchaguzi ya Malawi (MEC) iliomba siku 30 za ziada ili kura zihesabiwe upya kabla ya kutangaza matokeo.

Hata hivyo, Mahakama Kuu ilitupilia mbali ombi hilo na kutoa amri ya matokeo kutangaza siku ya Ijumaa.
"Sheria iko wazi, hakuna kuongeza muda," amesema Jaji Kenyatta Nyirenda.

Bwana Mutharika ni ndugu yake Rais Bingu wa Mutharika aliyefariki dunia mwaka 2012. Peter Mutharika alikuwa Waziri wa mambo ya nje wakati ndugu yake akiwa rais.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top