Daniel Agger
Na. Paul ManjaleKlabu ya Fc Barcelona iko katika mawindo makali kwa ajili ya kupata mlinzi mpya atakayekuja kuzipa pengo la mkongwe Carles Puyor anayeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Kati ya majina yanayotajwa kuja kurithi mikoba ya Puyor ni mlinzi wa Liverpool na nahodha wa timu ya taifa ya Denmark Daniel Agger (29).
Agger ambaye ni mlinzi wa zamani wa klabu ya Brondby IF ya nyumbani kwao Denmark amekuwa akiwindwa na klabu ya Barcelona kwa misimu kadhaa sasa.
Mwaka 2013 klabu ya Barcelona ilishuhudia ofa yao ya £17m ikitupiliwa mbali na klabu ya Liverpool kwa madau kuwa mlinzi huyo shupavu na mwenye nguvu za miguu hauzwi.
Hivi karibuni kituo cha Catalan Daily Sport kiliendesha upigaji kura kwa mashabiki ili kujua ni mlinzi yupi wanayetaka awe mrithi namba 1 wa Carles Puyor??
Mlinzi wa Chelsea David Luiz alipata kura 68 akifuatiwa na kinda wa kifaransa anayekipiga na klabu ya Atletico Bilbao Aymeric Laporte (19) aliyepata kura 29 huku Daniel Agger akiambulia kura 3 pekee.
Hii inamaanisha mashabiki wa klabu ya Barcelona wameukabidhi moyo wao kwa mbrazil David Luiz na siyo Daniel Agger.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.