Unknown Unknown Author
Title: LVG HAWATAKI KROOS, FABREGAS, NIA KWA WAWILI WA FEYENOORD & STROOTMAN!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
ZIMEZAGAA ripoti huko Ulaya kwamba Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal hana nia ya Toni Kroos wa Bayern Munich na Cesc Fabrega...
Louis van Gaal
ZIMEZAGAA ripoti huko Ulaya kwamba Meneja mpya wa Manchester United Louis van Gaal hana nia ya Toni Kroos wa Bayern Munich na Cesc Fabregas na badala yake anawataka Wachezaji wa Uholanzi ambayo ndie Kocha wa Timu ya Taifa.

Akiwa Kambini pamoja na Timu ya Holland inayojitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza huko Brazil hapo Juni 12, imedaiwa Louis van Gaal anataka kuwachukua Wachezaji wawili walioko Kambini humo wanaochezea Klabu ya Feyenoord, Jordy Clasie and Bruno Martins Indi, ili wajiunge nae Old Trafford mara baada ya Kombe la Dunia.
Kevin Strootman
Pamoja na hao, pia inasemekana LVG anamtaka Mchezaji wa AS Roma, Kevin Strootman, licha ya kuwa sasa yupo muda mrefu nje ya Uwanja akiuguza Goti lake badala ya Kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas.

Watatu hao, Clasie, Indi na Strootman, ni Waholanzi wenye sifa kemkem za umahiri mkubwa kiasi ambacho LVG sasa ameuagiza Uongozi wa Man United uanze mazungumzo Klabu zao na kumaliza kazi ya Uhamisho wao kimya kimya ili isije ikaonekana kama yeye, ambae ni Kocha wa Uholanzi, ametia mkono wake.
Jordy Clasie and Bruno Martins Indi,
Indi na Clasie, wote wakiwa na Miaka 22 kila mmoja, wamejipatia sifa kubwa Klabuni kwao Feyenoord kiasi ambacho Clasie Msimu huu amelazimika kuchukuliwa Timu ya Taifa ya Holland na pia Nahodha wa Holland, Robin van Persie, ambae pia ni Mchezaji wa Man United, kukiri Clasie ni Paul Scholes mpya.

Nae Bruno Martins Indi, Sentahafu Mrefu, mwenye nguvu na akili, ni nguzo imara ya Feyenoord na Holland.
>>Soka in bongo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top