Unknown Unknown Author
Title: DIEGO COSTA HUENDA AKAKOSA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA HAPO JUN 12, 2014
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KOCHA wa Mabingwa wa Dunia Spain, Vicente del Bosque, ameihakikishia Nchi yake kuwa hatachukua Mchezaji ‘Majeruhi’ kwenda huko Brazil kut...
Diego Costa
KOCHA wa Mabingwa wa Dunia Spain, Vicente del Bosque, ameihakikishia Nchi yake kuwa hatachukua Mchezaji ‘Majeruhi’ kwenda huko Brazil kutetea Taji lao la Ubingwa wa Dunia wakati Fainali za Kombe zitakapoanza Juni 12 lakini amejiweka njia panda kuhusu kumchukua Mbrazil Diego Costa kwani Straika huyo ni Majeruhi.
Wakati kila Nchi inatakiwa kuwasilisha Vikosi vyao vya Wachezaji 23 kwa FIFA ifikapo Juni 2, uwezekano wa Mbrazil Diego Costa alieikana Nchi yake ya Kuzaliwa ili aichezee Spain Kombe la Dunia huko Brazil, umekuwa finyu baada Daktari Jana Jumatatu kuamua Mchezaji huyo hatakiwa kucheza kwa Siku 15 ili kupona Musuli ya Pajani [Hamstring] iliyochanika kwa Kiwango cha Daraja la Kwanza.
Mara baada ya Jumatatu kupimwa kwenye Kliniki ya Cemtro huko Jijini Madrid, Dokta Pedro Guillén alithibitisha kuumia huko kwa Costa huku akionya tatizo la aina hiyo hujirudia hasa baada ya yeye kuchanika sehemu mbili zilizokaribiana.
Wikiendi iliyopita Klabu yake Atletico Madrid, ikicheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Real Madrid na kufungwa 4-1, ilichezea ‘Shilingi Chooni’ pale ilipoamua kumwanzisha Diego Costa kwenye Fainali hiyo huku akiwa na tatizo hilo hilo la Musuli za Pajani na matokeo yake alidumu Dakika 9 tu Uwanjani na kutolewa baada kujirudia tatizo hilo hilo.
Spain watacheza Mechi yao ya kwanza ya KUNDI B huko Brazil dhidi ya Holland hapo Juni 13 na ni wazi Diego Costa hatakuwa fiti.
Jumapili, Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, alisisitiza hatachukua Mchezaji asie fiti kwa Asilimia 100 kwenda Brazil na hilo ndio lilipelekea Costa kupimwa Jumatatu.
Hata hivyo, Costa hayumo kwenye Kikosi cha Spain kinachocheza Mechi ya Kirafiki dhidi ya Bolivia hapo Ijumaa Mei 30 huko Seville kwa vile Wachezaji wa Real Madrid na Atletico Madrid wamepumzishwa.
Kukosekana kwa Costa kwenda Brazil sasa kunafungua njia kwa Del Bosque kuchukua Mastraika Watatu kati ya Fernando Torres, David Villa, Álvaro Negredo na Fernando Llorente.
KOMBE la DUNIA :: RATIBA-Mechi za Ufunguzi:
[Saa za Bongo]
Alhamisi 12 Junii 2014
KUNDI A
2300 Brazil V Croatia
Ijumaa 13 Junii 2014
1900 Mexico V Cameroon
KWA RATIBA KAMILI BOFYA HAPA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top