HATIMAE GIRLFRIEND WA SAMIR NASRI AOMBA RADHI

Na. Paul Manjale
Mwanamitindo Anara Atanes ambaye ni mpenzi wa kiungo wa kifaransa Samir Nasri amejirudi na kuiomba radhi nchi ya Ufaransa.

Hii imekuja siku chache baada ya mwanamitindo huyo kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter...

F***France,F***Deschamps!!What a f***manager
Kufuatia Samir Nasri kuachwa katika kikosi kitakachokwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Anara anasema "Naomba radhi kwa yoyote niliyemkosea kutokana na kauli yangu kupitia tweeter sikumaanisha Ufaransa kama taifa.Hasira zangu zilikuwa zimelenga kwa Deschamps na siyo nchi"

Hii ni mara ya pili kwa Samir Nasri kuachwa katika hatua kama hizi za kuelekea kombe la dunia mara ya kwanza ikiwa ni huko bondeni(Afrika Kusini) mwaka 2010 na aliyekuwa kocha timu hiyo Raymond Domenech.

Wakati huohuo Nasri kuna habari zinasema Nasri anapanga kuachana moja kwa moja na timu ya taifa. Anasema "kwakweli inauma sana hii ni mara ya pili naachwa bila ya sababu za msingi utafika wakati nitanyoosha mikono juu na kusema inatosha sasa" Hili nililijua tangu mwanzo nikajiandaa kiakili,Unapompigia kocha simu ili umuombe msamaha anagoma kupokea unategemea nini?bila shaka hakutaki.....

Je, Deschamps anasemaje?Deschamps "Nasri ni mchezaji muhimu kwa Manchester City lakini siyo kwa Ufaransa.Ni mchezaji ambaye haridhiki kukaa benchi hivyo hafai kuwemo kikosini kwangu"...

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post