Diamond Platnumz akiwasili katika Studio za Safari Radio kwa ajili ya Mahojiano ya Moja kwa moja Kupitia kipindi cha Boda Boda, akiwa ameongozana na Wema Sepetu, Martin Kadinda pamoja na Babu Tale na RomyJones na Bausa wake. Diamond Platnumz atafanya show kubwa leo hii pale Makonde Beach ikiwa ni kwa udhamini wa Vodacom, Naf Beach Hotel, Safari Radio na Lindi Yetu Blog.
Wema Sepetu akiweka Sahihi katika Kitabu cha kumbukumbu cha wageni Baada ya Kuwasili katika Studio za Safari Radio Mtwara akiwa na Ubavu wake Diamond Platnumz.
Diamondi Platnumz akizungumzia Jinsi Show yake itakavyo kuwa pale Makondo Beach Leo hii, amewaahidi wakazi wa Mtwara kuwa itakuwa ya Tofauti sana kuliko show zote alizowhi kufanya hasa yuko na Baby wake so hataki kumuangusha katika hilo, hivyo amewaomba kujitokeza kwa wingi ili usiweze kuikosa.
Wema Sepetu akizungumza live kupitia 89.9 fm Safari radio Mtwara kuhusiana na ujio wake katika Show hiyo ya baby wake Diamond Platnumz na kuwaahidi kuwepo kwa Suprise Nyingi kwa wale watakao jitokeza katika Show hiyo ya Kihistoria Mkoani Mtwara.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kusini akizungumzia ujio wa Diamond Platnumz mkoani Mtwara na wao kama wadhamini wanasapoti mziki wa Kizazi Kipya na wasanii wa Tanzania nddio maana wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kudhamini Show hiyo ya Msanii huyo Mkoani humo.
Picha ya Pamoja Crew ya Safari Radio na Diamond Platnumz na Wema Sepetu
Diamond Na Wema walipata Kufanya Mahojiano pia ya Live kupitia Mtwara Cable Television na Host wao kama waonekanavyo hapo juu kwenye picha.
Baada ya Mizunguko ya Interview nyingi aliwasili katika Hoteli ya Naf Beach kwa ajili ya Mapumziko tayari kujiandaa na Show hiyo mida ya Kuanzia saa 7:30pm pale Makonde Beach.
Akiwa na Mmoja wa Fans wao mtoto huyu ambaye walikutananae Hotelini hapo na Kuweza Kushow Love kwa kupiga picha ya Pamoja.
Crew ya Safari Radio inakuambia Hii si ya Kukosa ni Show ya Kihistoria Jisogeze Pande za Makonde Beach.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.