BABY MADAHA AUMBUKA ASHINDWA KUTEKELEZA AHADI KWA MASHABIKI WAKE, SOMA HAPA

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ambaye aliwahi kutangaza kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta akiumbuka kwa mashabiki wake kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu kwa kuachia kazi mpya na kuandaa matamasha mbali mbali.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akiwa kwenye pozi.
Msanii huyo alitoa uamuzi huo kwa madai kuwa alichoshwa na skendo za kila kukicha ambazo wakati mwingine zimekuwa zikimshushia hadhi katika jamii, ikiwemo skendo ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza ilioandaliwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post