ANGALIA KIPANDE CHA VIDEO MPYA YA WIMBO MPYA "SUBIRA" WA MSANII SHAA, MAUNO YALIYOMO NI HATARII....!!!!

Sara new video
Akiwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina yao Tanzania na hata kwenye nchi jirani, mwimbaji Shaa atarudi tena kwenye spika zako na kwenye TV yako hivi karibuni akiwa na sound mpya ya single yake ambayo mazingira ya kiswahili/Kitanzania yamehusika ndani yake.

Hii ni May 18 2014 wakati akiifanya video ya single hii iitwayo ‘subira’ maeneo ya Manzese Dar es salaam kupitia mikono ya Director anaepewa heshima kila siku kutokana na mikono yake kuhusika kuzipeleka mbali video za kitanzania…. Adam Juma kutoka Next level.

Wakati ukiwa tayari kupokea video mpya unaweza kutumia sekunde zako kucheki jinsi utengenezwaji wenyewe ulivyofanyika kisha uache maoni yako.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post