Unknown Unknown Author
Title: WIMBO WA BABY MADAHA “NICE AND SLOW” WATAJWA KUWANIA MTV EUROPE AWARDS
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wimbo wa Baby Madaha uitwao ‘Nice and Slow’ umechaguliwa kuwania tuzo za MTV Europe mwaka 2014. Msanii huyo wa Candy n Candy Records, ameia...

clip_image001Wimbo wa Baby Madaha uitwao ‘Nice and Slow’ umechaguliwa kuwania tuzo za MTV Europe mwaka 2014. Msanii huyo wa Candy n Candy Records, ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa anasuburi kutumiwa code kwaajili ya kuuwezesha wimbo huo kupigiwa kura.“Nilitoa song inaitwa ‘Nice and Slow’ ni whisper song (wimbo wa kunong’oneza) haiendani na mazingira ya kitanzania. Kwahiyo nikawa nimeipeleka moja kwa moja kwenye reverbnation chart, nilivyoipeleka UK kwasababu unajua Joe, huyu meneja wa Candy n Candy, ile kampuni tuliyoingia nayo ubia wa kusambaza movie pia wanasambaza muziki. Kwahiyo walipoisambaza UK ikawa imeingia kwenye chart za reverbnation, sasa hivi ipo namba mbili. Kwahiyo ni wimbo pekee kutoka Afrika ambao umefanya poa especially Afrika Mashariki,” amesema.

Kwahiyo kwenye group ya upcoming artists, MTV wameniandikia barua wakaniambia ‘umekuwa nominated, usubiri code kwaajili ya kupigiwa kura.”

Katika wimbo huo, Baby Madaha amemshirikisha bosi wake, Joe Kairuki ambaye ni CEO wa label hiyo. Hata hivyo akiongea na gazeti la The Star la Kenya, Kairuki alidai kuwa ili wimbo huo uingie kwenye kinyang’anyiro cha mwisho ni lazima upigiwe kura 2000.

“All we are urging our fans is to vote highly for the song once it’s put up for voting this Friday. the song must amass 2000 or more votes in order to be nominated for the awards and we hope our fans will not let us down,” alisema.

Muimbaji huyo amesema pia kuwa wimbo huo umetajwa kuwania tuzo zingine ziitwazo International Music Entertainment Awards, IMEA.

“Tuzo nyingine ni IMEA so nasubiri code ili kura zianze. Naomba watu waniunge mkono niipaishe Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. I am so happy for that kupiga hatua kimataifa,” ameongeza.

Msikilize zaidi hapa.

>>BONGO5.COM

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top