Baada ya ukimya wa takriban miezi 7 toka alipoachia ‘Tupogo’ mwaka jana, Ommy Dimpoz anatarajia kutoa single yake mpya iitwayo ‘Ndagushima’ mwezi huu.Dimpoz amesema wimbo huo utatoka wiki mbili zijazo ikiwa ni audio pamoja na video ambayo ameshoot nchini Uingereza hivi karibuni.
“Sasa hivi nakuja na ujio mpya nyimbo inaitwa Ndagushima ni Kiha cha Kigoma ambacho amenisaidia Linex kupata wazo la hiyo kwa sababu nilikuwa anataka kuweka maneno kidogo ya Kiha” Amesema Dimpoz leo kupitia Power Jams ya EA Radio.
Ommy amesema Ndagushima Chane maana yake ni Nakupenda sana.
Akijibu swali la shabiki kupitia Kikaangoni Live ya ukurasa wa EATV aliyetaka kujua kuhusu lini video ya Tupogo itatoka, Ommy amesema “ratiba za jmartins na zangu zimekuwa zinapishana sana tukipata nafasi tutashoot ila natoa video mpya mwezi huu”.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.