Unknown Unknown Author
Title: WASANII... ISABELA NA KALAMA WAMWAGANA...KISA?! SOMA ZAIDI HAPA..
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda 'Bella' na Kalama Bakari ‘Luteni’ wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya G...
Wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda 'Bella' na Kalama Bakari ‘Luteni’ wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Global TV Online hivi karibuni  kabla ya kumwagana.

Chanzo makini kilicho karibu na nyota hao wawili, kilisema kuachana kwao kunatokana na Luteni Kalama kukosa uaminifu kwa mwenzake kwani mara kadhaa, Isabela alizifuma meseji za wanawake wengine kwenye simu yake.
 

Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ memba wa Kundi la Gangwe Mobb katika pozi.
Kana kwamba haitoshi, Kalama ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mobb, pia hivi karibuni, licha ya kutotokea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Isabela, lakini alishindwa hata kumtumia ujumbe wa kumtakia heri. 

“Ni kweli nimeamua kujiweka pembeni kwa sababu Kalama siyo mwaminifu, nilikuta meseji mbalimbali za mapenzi za wanawake wengine, naogopa Ukimwi, bora nikae pembeni nimuache aendelee kufanya umalaya wake maana huyu ni sikio la kufa,” alisema Isabela baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa habari hizo. 

“Kilichoniumiza zaidi, hivi karibuni ilikuwa bethidei yangu hata hajani-wish kunijulia hali wakati nilikuwa ninaumwa, bora niendelee na maisha yangu, ndiyo maana mmeona hata kwenye uzinduzi wa Global Tv kila mtu alikuja kivyake.” 


Kalama alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Mimi sijui kama tumeachana, lakini kama Isabela ameamua hivyo ni sawa tu, ninachojua kila mtu yupo kwake, mimi niko Tabata yeye Kijitonyama.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top