Unknown Unknown Author
Title: MWANAMKE ALIYECHOKA KUISHI ASAIDIWA KIFO AKIWA NA MIAKA 99
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamke wa pili wa Kiingereza ambaye 'alichoka kuishi' amesaidiwa kufa kwenye kliniki ya kujitoa mhanga nchini Uswisi. Mwanamke huy...
Mwanamke wa pili wa Kiingereza ambaye 'alichoka kuishi' amesaidiwa kufa kwenye kliniki ya kujitoa mhanga nchini Uswisi.

Mwanamke huyo, ambaye alikuwa na umri wa miaka 99 akitokea London, hakuwa mgonjwa au mwenye ulemavu na kwa kifupi alichagua kusitisha maisha yake.

 
Tukio hilo limekuja baada ya mwalimu mstaafu kujiua kwenye kliniki ya Dignitas nchini Uswisi baada ya kushindwa kuendana na kasi ya maisha ya kisasa na jinsi ambavyo teknolojia iilivyokuwa ikiibadilisha jamii.

 
Mwanamke huyo mwenye miaka 89 alidhani kwamba afya yake dhoofu, pamoja na imani yake kwamba watu wamegeuka 'maroboti' waliofungwa kwenye vifaa vyao, walimpa sababu kidogo za kuishi.

 
Mwanamke huyo, ambaye alitaka afahamike tu kama Anne, alikuwa akisumbuliwa na kuzorota kwa afya yake katika miaka ya karibuni, lakini hakuwa akiugua ama udhaifu.
Vifo hivyo vimezua midahalo kuhusiana na uwiano wa haki ya kufa dhidi ya hatari ambazo watu wasio salama wanaweza kuzikabili.

 
Daktari mstaafu Michael Irwin ameshawasaidia Waingereza wengi kukatisha maisha yao kwenye kliniki za kujitoa mhanga za Uswisi. Alisema kwamba wagonjwa 3,000 husaidiwa kukatisha maisha yao kila mwaka.

 
Alisema: "Madaktari hawatamani kusimama na kutazama wagonjwa wakiteseka bila msaada. Mara zote imekuwa ikiendelea."

 
Alisema kwamba mwanamke wa pili hakufanya hivyo Dignitas, lakini badala yake alikwenda kwenye kliniki ndogo zaidi.

 
Alisema: "Hakuwa mgonjwa mahututi, wala kuwa na ulemavu wowote, isipokuwa hakuweza kabisa kupata raha katika maisha na kudhani ni wakati mwafaka kusema kwaheri."

 
Dokta Irwin ndiye aliyeanzisha taasisi ya Society for Old Age Rational Suicide na kusaidia maombi ya Anne kwenda Dignitas.

 
Anne alipokuwa mtu mzima na majukumu yake ya kila siku kuendelea kumbana, aliamua kwenye kliniki ya Dignitas.
Dokta Irwin alisema kulikuwa na takribani watu watatu wenye matatizo yanayofanana na ya Anne ambao walikatisha maisha yao nchini Uswisi katika miaka ya hivi karibuni.

 
Kunatakiwa kuwe na kura huru katika Bunge kuhusiana na Muswada wa Kusaidia Kifo, ambapo madaktari wawili wanaweza kupendekeza dozi ya kifo ya vidonge kwa mgonjwa mahututi kabisa aliyebakisha miezi isiyozidi sita ya kuishi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top