Unknown Unknown Author
Title: MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANANCHI WA MKOA WA LINDI KUKUBALI MFUMO WA SERIKALI MBILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete leo hii amezungumza na wananchi wakazi wa Mnazi mmoja Mkoa wa Lindi kati...
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete leo hii amezungumza na wananchi wakazi wa Mnazi mmoja Mkoa wa Lindi katika Ziara ya kichama ya Kudumisha muungano wa Tanzania.

Katika mkutano huo wa Hadhara Mama Salma Kikwete amewaomba wananchi kuikubali rasimu ya katika Kwa muundo wa Serikali mbili kwani Serikali Tatu ni mzigo na Gharama kubwa kwa Taifa na Pia ilikulinda Muungano uliowekwa na waasisi wa Taifa hili Muundo wa Serikali Mbili ndio jawabu sahihi la sivyo Muungano wetu Utavunjika.

Mama Salma ametoa hutuba yake fupi leo hii kwa wakazi hao wa Mnazi mmoja kwa lugha ya Kimwera na kufanya wananchi waliofika katika Mkutano huo kuweza kumpigia makofi mara kadhaa wakati wa mazungumzo yake hiyo inaashiria kumuelewa zaidi nini alikuwa anazungumza na nini alikuwa anahitaji wakifanye wao. 

Lakini kwa wale watu wasio wazawa najua watakuwa wametoka kapa (yaani bila kuelewa).

Awali Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Lindi ndg Amiri Mkalipa aliwataka vijana kutumia fulsa zilizopo kujiletea maendeleo na bila kusahau kushiriki katika kugombea viti mbalimbali wakati wa Uchaguzi utakapofika bila ya woga wowote kwani taifa ndilo linawategemea kuliendeleaza.

Ziara hiyo ilikuwa na Kauli mbiu ya "KULINDA NA KUENZI MUUNGANO BILA UBAGUZI WA AINA YOYOTE", Matembezi hayo yaliyoanzia Mjini Dodoma Kuzunguka Tanzania Nzima na Waendesha PikiPiki wa Vijana wa CCM ulipokelewa kwa Shangwe katika Manispaa ya Lindi Leo hii.
Mama Salma Kikwete akipokelewa mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika Viwanja vya Mnazi mmoja wakati wa Mapokezi ya waendesha Bodaboda kutoka UVCCM MKOA waliokuwa na ziara ya kuzunguka Mikoa kadhaa ya Tanzania na "Kuaulimbiu ya Kulinda Muungano Bila Ubaguzi wa aina yoyote ile".
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Wakazi wa wa Kijiji cha Mnazi Mmoja waliojitokeza katika Mapokezi hayo ya Waendesha Bodaboda ya UVCCM na Kaulimbiu yao ya "KULINDA NA KUENZI MUUNGANO BILA UBAGUZI WAINA YOYOTE" 
Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Nassoro Hamid akiteta jambo na Mmoja wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakati wa Mkutano wa hadhara wa chama hicho eneo la Mnazimmoja Lindi.  
Katibu wa CCM mkoa wa Lindi Ndg Adelina Gefu akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika Viwanja hivyo vya Miembesita Eneo la Mnazi mmoja Lindi. 
Mumbe wa baraza Kuu la Vijina la CCM Ndg JABIR OMAR akiwasalimu wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa Hadhara leo hii katika Viwanja vya Miembe sita Eneo la Mnazi Mmoja Lindi Mjini. 
Mwenyekiti wa UVCCM MKOA Ndg Amiri Mkalipa akitoa neno kwa wananchi waliohuddhuria Mkutano huo wa Hadhara mapema leo katika viwanja vya Miembesita Eneo la Mnazi mmoja Lindi Mjini. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi Ndg Mtopa Akiwasalimia wananchi waliohudhuria Hadhara hiyo mapema leo viwanja vya miembe sita Mnazi Mmoja.
Kikundi cha Burudani kikitoa Burudani wakati wa Hafla hiyo mapema leo hii. 
Wazee wakitumbuiza mbele ya mgeni rasmi mama Salma Kikwete wakati wa Mkutano wa hadhara mapema leo Viwanja vya Miembesita, Mnazi mmoja Lindi. 
Wananchi wakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinazungumzwa katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi. katika Viwanja vya Miembesita, Mnazi Mmoja Lindi. 
Mh. Diwani wa Kata ya Mingoyo Jamaldin Mandowa akifanya Ukodac wake katika Hadhara Hiyo mapema leo katika viwanja vya Miembesita Mnazimmoja Lindi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top