Unknown Unknown Author
Title: MAFIKIZOLO KUFANYA VIDEO YA WIMBO WAO MPYA “NAKUPENDA” TANZANIA NA DIRECTOR WA HAPA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ambalo lipo nchini kwajili ya show moja itakayofanyika leo Mlimani City, lina mpango wa k...

Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ambalo lipo nchini kwajili ya show moja itakayofanyika leo Mlimani City, lina mpango wa kufanya video ya wimbo wao mpya ‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya kuondoka.

MAFIKIZOLOTheo Kgosinkwe and Nhlanhla Nciza.

“Tungependa kufanya video ya Nakupenda hapa Dar kwani jina la wimbo ni la kiswahili na itapendeza hivyo, bado hatujapata director wa kufanya video hii ila ndio mpango wetu”waliiambia Sammisago.com

Pia Mafikizolo wamesema wamefanya mabadiliko makubwa katika muziki wao ili kukidhi haja za bara zima la Afrika.

“mabadiliko ya muziki wetu yalifanyika ili kuteka soko la bara lote la Africa na zaidi ikiwezekana ndio maana Khona na Happiness zina miondoka tofauti”. Alisema Nhlanhla Nciza

Katika hatua nyingine Mafikizolo wamethibitisha kuwa wanampango wa kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka Tanzania atakaye tajwa hivi karibuni na collabo hii ndio chanzo cha kuboresha mahusiano mazuri na wasanii wa Tanzania.

>>Sammisago.com

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top