JE WAJUA SABABU YA HEMEDY PHD KUANDIKA WIMBO "ON MY WEDDING DAY"..? SOMA HAPA KUJUA UNDANI ZAIDI

Girlfriend wa Hemedy
Hemedy PHD amesema girlfriend wake aliyemtambulisha wazi ndiye aliyemvutia kuandika wimbo wake ujao uitwao ‘On My Wedding Day’.

Amesema amekuwa akifuatilia maisha ya mastaa wa nje na kugundua kuwa wengi wamekuwa wakiyaweka wazi mahusiano yao tofauti na wasanii wa Tanzania na ndio maana naye ameamua kumweka wazi na kuwa huru. 
“Kwasababu ni demu ambaye nina uhakika naye, demu ambaye moyo wangu naona kabisa umependa nikapata mpaka mawazo kwamba one day nahisi huyu ndiye atakayekuja kuwa one and only wa kumuoa ndio hiyo idea ya kuandika hiyo ngoma ikaja,” amesema.


Hemedy ameongeza kuwa ameandika wimbo huo kwakuwa anaamini kuwa harusi ni sherehe zilizopo katika maisha yote ya binadamu na hivyo kama ukipendwa unaweza kumletea neema. Amesema pia kuwa mashabiki wake wategemee video ya tofauti sana ya wimbo huo na hadi sasa amekuwa akiumiza kichwa namna ya kuifanya isiwe ya kawaida.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post