GAZETI LA MAWIO LAPEWA SIKU TATU LIJIELEZE NA SIKU 7 ZA KUKANUSHA HABARI WALIYOITOA. NI KUHUSU HATI YA MUUNGANO

Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano.

Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.
Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23, mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.

Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,” alisema. 

Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post